Sakinisha
Swa ina njia moja ya kujenga: mfululizo safi wa Swa, bila gcc, ld, clang, libc, Rust wala LLVM.
Njia ya 1 — Mfululizo safi wa Swa
Hii ndiyo njia ya uzalishaji. Mahitaji: x86-64 Linux na bash pamoja na zana za kawaida za mfumo (cat, cmp, chmod, mktemp, timeout, grep, md5sum). Hakuna Rust, hakuna LLVM, hakuna clang, hakuna libc popote kwenye mfululizo huu.
Kuanza — chanzo cha uaminifu
Mfululizo unaanza na Kwanza, programu ya baiti 393 za mkono iliyoandikwa bila lugha nyingine yoyote. Kizinduzi kidogo cha mkono kinatumia Kwanza pekee kujenga upya mjenzi, awali (msingi/awali.bin) na kizinduzi chenyewe kutoka vyanzo vyao, na kuthibitisha kila kimoja ni sawa kwa baiti na kilichohifadhiwa — bila NASM wala kiunganishi:
git clone https://github.com/lugha-swa/swa.git
cd swa
./msingi/kizinduzi.bin gharama/mwanzo.kizinduzi
Mkusanyaji wa Swa
Mapishi moja yanaendesha mfululizo mzima: baiti 393 → kusanyiko → awali → msuluhishi wa husisha (hujengwa na awali) hutatua utegemezi wa msingi/mkusanyaji/kiendeshaji.swa → awali inakusanya mkusanyaji kamili → mkusanyaji kamili hujijenga upya kuwa bin/swa. Kila hatua ni ELF tuli (bendera --programu), bila kiunganishi:
./msingi/mjenzi.bin gharama/jenga.mapishi
Programu yako ya kwanza
Programu hukusanywa kwa bin/swa. Maktaba ya msingi huingizwa kwa husisha — mkusanyaji hufuata utegemezi wenyewe, kwa mpito. Njia za husisha ni kutoka saraka kuu ya hazina ya swa, kwa hiyo endesha amri ukiwa hapo. Andika programu hii kwenye faili salamu.swa:
husisha { msingi/maktaba/kumbukumbu.swa }
n32 anza() {
andika("Habari, Swa!\n");
rudisha 0;
}
bin/swa --programu salamu.swa > salamu
chmod +x salamu
./salamu
Majaribio kamili ya mfululizo
Mapishi moja yanaendesha majaribio yote ya mfululizo: programu za majaribio/programu/ORODHA.txt kwenye mifululizo yote miwili (awali na mkusanyaji kamili), uthabiti (mkusanyaji hujijenga mara mbili, na matokeo mawili ni sawa kwa baiti), mkazo wa urekebishaji wa wito 1,000 wa mbele, desimali, na kujiumbiza kwa kipanga umbizo. Hakuna Rust, hakuna LLVM, hakuna clang:
./msingi/mjenzi.bin gharama/jaribu-mfululizo.mapishi
Dereva wa zamani wa Rust/LLVM
Hadi 2026-09-05 kulikuwa na dereva wa majaribio wa Rust/LLVM. Umehamishiwa hazina ya kumbukumbu lugha-swa/swa-dereva na haujengwi tena; hazina kuu ya Swa ina lugha moja tu: Swa.
Jukwaa linaloungwa mkono
- x86-64 Linux ndilo jukwaa pekee la uzalishaji.
- ARM64 na RISC-V hazijaungwa mkono bado. Kila usanifu ni mradi wake: unahitaji baiti mpya za mkono za Kwanza, kizalishe kipya cha awali, na ABI ya jukwaa.
- Windows haijaungwa mkono — kizuizi cha BSS bado hakijatatuliwa.
- Zana ambazo bado hazipo: LSP, debugger, na kidhibiti cha vifurushi. Kipanga umbaji kipo (zana/umbizaji.swa).